Neno “Narcolepsy” (hali ya kusinzia hasa mchana) linalotokana na neno “Narcolepsie” ambalo ni neno la Kifaransa. Neno hilo la Kifaransa — narcolepsie, lilitumika kwa mara ya kwanza mnamo wa mwaka 1880 naye Jean Baptiste kwa wakati huo alitumia maneno ya Kigiriki; vapka maana yake “kukufa ganzi” na “lepsie” maana yake shambulio la neva
Neva — Nervus (latin) nerves — English
Maelezo muhimu kuhusu Nakolepsi (shambulio la neva la usingizi)
Nakolepsi ni hali sugu ya neva ambayo huharibu/hudhoofisha uwezo wa ubongo kudhibiti usingizi na kuwa macho. Unaadhiri takribani mtu mmoja (1) kati ya watu elfu mbili (2,000) — watu milioni tatu (3) dunia nzima.
Dalili za Nakolepsi
Mwanzo wa ugonjwa wa narcolepsy unaweza kutokea wakati wowote kati ya utoto wa mapema na umri wa miaka 50. Vipindi viwili vya wakati wa kilele vimetambuliwa; mmoja karibu na umri wa miaka 12 na mwingine karibu miaka 36. Watafiti wengine wanaamini kuwa ugonjwa wa narcolepsy haujulikani sana kwa watoto. Nakolepsi huelekea kubaki hali ya maisha yote.
Dalili hizi huwa tofauti kutoka mtu mmoja hadi mwengine.
Usingizi wakupindukia hasa mchana
Vipindi vya usingizi mwingi wakati wa mchana zikilinganishwa na jinsi mtu asiye na Nakolepsi angehisi akiwa macho kwa masaa 48 -72 (arobaini na nane mpaka sabini na mbili) mara nyingi husababisha ugumu wa kuwa makini na kutahadhari,
Udhaifu wa misuli
Vipindi vya ghafla vya kudhoofika kwa misuli kutokana na hisia kama vile kicheko, uchangamfu, kushangaa au kukasirika. Makali yake huwa tofauti, pengine kuregea kwa taya au kudhoofika kwa magoti hatimaye kuanguka chini. Hili linaweza tendeka kwa sekunde hadi madakika kadhaa ndiposa muadhiriwa apate fahamu zake kamili (ingawa anaewezadhindwa kuongea) katika kipindo kile
Ndoto (Kuota njozi)
Ndoto pindi tu alalapo na mar utu aamkapo. Ndoto hizi zinaweza kuhusisha taswira, kusikia au kugusa.
Kupooza usingizini
Kutoweza kusonga kwa sekunde au dakika chache pindi tu mtu alalapo au maratu aamkapo. Mara nyingi ndoto (kuota njozi) za kabla na baada ya kulala hufuatia.
Kuvurugika kwa muda awa usingizi
Tofauti na mtazamo wa umma, watu wanaoadhirika na Nakolepsi hawalali kila wakati, mud awa kulala huzimwa, hivyo hupambana na kutolala mchana lakini usiku hupambana na kulala.
Kulala kidogo
ni kipindi kifupi cha kulala kidogo ambacho hufanyika ghafla na bila nia. Aina hii ya usingizi hufanyika wakati ubongo hubadilika bila kutarajia kati ya hali ya kuamka na kulala, na sehemu za ubongo zimefungwa. Kulala kidogo ni sehemu ya muda ya kulala au kusinzia ambayo inaweza kudumu kwa sekunde moja au hadi sekunde 30 ambapo mtu hushindwa kujibu maoni ya kiholela na huwa hajitambui.
Sayansi ya Nakolepsi
Kuna aina mbili ya Nakolepsi: Nakolepsi ikiwa na udhaifu wa misuli na Nakolepsi isyokuwa na udhaifu wa misuli. Ilyo sababishwa na ukosefu wa hypocretini, ambayo ni mtoaji wa neva muhimu inayo saidia uendelezaji wa umakini na kudhibiti hali ya kulala na kuamka.Kidogo kinajulikana kuhusu nakolepsi isiyokuwa naudhaifu wa misuli.
UTAMBUZI
Ikiwa unashuku kuwa wewe au mpendwa unaweza kuwa na dalili za ugonjwa wa narcolepsy, ni muhimu kushauriana na mtaalam wa kulala au mtaalamu wa magonjwa ya akili aliyethibitishwa na bodi.
Udhibiti
Matibabu yanapatikana leo na inaweza kuboresha dalili za ugonjwa wa nakolepsi. Udhibiti wa dalili hutofautiana sana na mtu na mara nyingi huchukua muda mrefu kupata mojawapo mchanganyiko wa matibabu.
Kuongeza ufahamu
Kwa sababu ya ufahamu mdogo na maoni potofu, kuna wastani wa miaka 8 hadi 15 kati ya dalili ya ugonjwa na mwanzo na utambuzi. Inakadiriwa kuwa wengi wa watu walio na ugonjwa wa nakolepsi kwa sasa hawajatambuliwa au kugunduliwa vibaya (utambuzi mbaya wa kawaida ni pamoja na kifafa, unyogovu na dhiki na Skizofrenia)
Shukrani za Mtafsiri Magdalene Aseyo